Rais Samia Amjibu Zitto Kabwe Kuhusu Msamaha wa Mbowe"




Katika Mkutano wa Wadau wa kujadili hali ya Demokrasia ya Vyama vyingi nchini Kiongozi wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amemuomba Rais Samia kwa kufuata sheria awezeshe Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aachiwe huru kwa nia ya kuleta muafaka wa kitaifa.

Rais Samia amemjibu Zitto Kabwe kama ifuatavyo:-

"Nataka nijibu lile ombi la mwanangu, iko hivi demokrasia ni kuheshimu sheria, unapoheshimu sheria ndipo demokrasia inapokua, lakini pia ndipo inapoleta heshima.

“Heshima ya mtu inakuja unapoheshimu sheria za nchi, unapovunja sheria za nchi heshima yako haitaheshimiwa, serikali haitakuheshimu lakini lazima ujue kwamba unapotumia uhuru wako mwisho wa uhuru wako inaanza heshima ya mtu mwingine.

"Isingekuwa uvunjifu wa sheria leo isingemlazimu Zitto kuomba hapa kwamba yule mwenzetu muachie lakini unapovunja sheria unajivunjia heshima

“Naomba tufanye kazi kwa kuheshimu sheria, waswahili wanasema mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba, ingawa kusameheana nako kupo"

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad