Rais wa Somalia amtimua waziri mkuu wake akimtuhumu kutaka kumpinuda




RAIS wa Somalia, anayemaliza muda wake, Mohamed Abdullahi Farmajo, amemsimamisha kazi Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mohamed Hussein Roble, ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana Jumapili, tarehe 26 Desemba 2021 na Ofisi ya Rais wa Somalia.

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, Roble anatuhumiwa kupanga mapinduzi yasiyo rasmi dhidi ya Rais Farmajo.

Huku wafuasi wa waziri mkuu huyo wa Somalia, akiwemo Msaidizi wa Waziri wa Habari nchini humo, Yusuf Omar Adala, aliyedai kuwa uamuzi huo wa Rais Farmajo, ni sawa na mapinduzi yasiyo ya moja kwa moja.


 
Inadaiwa kuwa, Rais Farmajo ametangaza kumsimamisha kazi Roble, siku moja tangu mwanasiasa huyo kumshutumu kwamba anakwamisha uchaguzi wa wabunge unaonedelea nchini humo.

Katika taarifa ya Ofisi ya Rais wa Somalia, imesema Roble ni tishio kwa mchakato wa uchaguzi huo, na kwamba anavuka mamlaka yake.

The outrageous statement from immediate former President, Mohamed Abdullahi (Farmajo) regarding the work of the PM & his failed attempt to militarily take over the OPM is a violation of the constitution & other laws, the consequences of which will be solely shouldered by Farmajo pic.twitter.com/P5gtkaiUsI


— SomaliPM (@SomaliPM) December 27, 2021

Hii ni mara ya pili kwa Rais Farmajo kutangaza kumsimamisha kazi Roble, ambapo mara ya kwanza alichukua hatua hiyo Mei 2021, kufuatia mgogoro wao kuhusu kukwama kwa uchaguzi wa wabunge.

Hata hivyo, Roble alijibu tuhuma hizo kupitia ofisi yake, akidai kwamba Rais Farmajo ndiye anayetumia nguvu kubwa na rasilimali fedha kuvuruga uchaguzi huo.

Kupitia taarifa yake, Roble alisema atafafanya mikutano kutafuta njia za kuharakisha uchaguzi huo .


 
Imeripotiwa kuwa, uchaguzi wa wabunge ulioanza Novemba Mosi mwaka huu, ulipaswa kufika tamati tarehe 24 Desemba 2021, lakini hadi sasa haujaisha huku wabunge 24 ndiyo waliochaguliwa kati ya wabunge 275 wanaotarajiwa kuchaguliwa.

Ukurasa wa Twitter wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia, leo Jumatatu imeandika ukidai kuwa, uamuzi wa Rais Farmajo kumsimamisha kazi Roble unakiuka katiba ya taifa hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad