December 13,2010 tasnia ya muziki tokea Tanzania ilimpoteza mkongwe wa muziki wa dansi, Dr. Ramadhan (Remmy) Mtoro Ongala akiwa na umri wa miaka 63, na siku ya Jana,Dec 13 ametimiza miaka 11 toka kuondoka kwake ambapo alifia nyumbani kwake Sinza (mtaa uliopewa jina lake SINZA KWA REMMY) kwa maradhi ya kisukari. Ana historia ndefu na yenye kuvutia,ubaya haiwezi malizika leo wala kesho.
Kabla ya kuzaliwa kwake, mama yake mzazi alibeba mimba mbili ambazo ziliharibika,alipo beba ujauzito wa Remmy ikabidi aende kwa mganga,na akaambiwa akajifungulie Maporini na mtoto akizaliwa hasithubutu kumnyoa nywele kwenye maisha yake yote. Dr. Remmy alizaliwa akiwa na meno mawili,jamii ikamtabiria kuja kuwa mganga mkubwa sana huko kwao, Zaire na utabiri haukutimia bali akaja kuwa mwimbaji mkubwa nchini na Afrika kiujumla, na hapo inasemekana kwa kuwa alitabiriwa uganga basi Ndiyo sehemu Jina la DR. REMMY likaibukia hapo.
Aliwahi kudai majaji wamemuhujumu kumyima tuzo ya mshindi mwenye sura mbaya Tanzania ambapo alikamata nafasi ya pili kwenye shindano hilo lililofanyika kinondoni Dar es salaam na mshindi akiwa Masoud Sura mbaya na wa tatu akiwa MZEE JANGALA, wakati Remmy anaamini yeye ndiye mtu mwenye sura mbaya kuliko wote, Masoud alisema hata wakienda kukata rufaa hawamzidi kwa kuwa na sura mbaya na atawashinda tena.
Remmy anabaki kwenye kumbukumbu kubwa za kuwa mtu wa kwanza nchini kuthubutu kukemea hadharani ngono zembe akitunga wimbo uliyoitwa mambo kwa soksi,jamii na serikali ilimbeza ikiamini wimbo huo haukuwa na maadili,hadi pale ilipokuja kueleweka wimbo ulimaanisha nini,viongozi wa dini na serikali wakaanza kuhubiri mambo hayo wakitumia wimbo huo.
Kipenda roho ni wimbo aliomuimbia mkewe Mzungu,akiamini Mapenzi sio sura maana kama ni sura,yeye ni miongoni mwa watu waliojaliwa Sura mbaya duniani lakini akaoa mrembo wa kizungu, Pia Dr. Remmy alikuwa na gari baya kiasi kwamba kila lilipokatiza watu walishangaa,akaenda kuandika maneno BABA YAKO ANALO 🤣?
Akiwa na Band ya Super Matimila walitoa hits kibao zilizofanywa chini ya studio za Real World,uingereza. inaendelea kwenye comment