Rufaa ya kina Sabaya kuanza kusikilizwa Februari



Arusha. Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha imepanga kuanza kusikiliza rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili Februari 14, 2022.


Sabaya kupitia mawakili wake wamekata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Oktoba 15 mwaka huu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.


Wakata rufaa akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wakisubiri kutajwa kwa Rufaa yao katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha leo Jumatatu Desemba 13, 2021. Picha na Picha na Janeth Mushi.


Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Ruth Massam amesema leo Desemba 13, 2021 rufaa hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kuanza kusikiliza.


Amesema rufaa hiyo itakayosikilizwa mfulululizo itaanza Februari 14 mwakani mbele ya Jaji atakayekuwa amepangiwa.


"Leo imekuja kwa ajili ya kupanga tarehe ya kuanza kusikilizwa. Itaanza kusikilizwa Februari 14, 2022 mbele ya Jaji atakayepangiwa na itaendelea mfulululizo kama mtakavyoelekezwa,"amesema


Rufaa hiyo namba 129 ya mwaka huu, wajibu Rufaa (Jamhuri), waliwakilishwa na jopo la mawakili wanne wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Tumaini Kweka, Mawakili wa Serikali Waandamizi Ofmed Mtenga, Felix Kwetukia na Wakil wa Serikali Baraka Mgaya.


Waomba rufaa ambao ni Sabaya, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, waliwakilishwa na Mawakili Mosses Mahuna, Sylvester Kahunduka na Fauzia Mustapha.


Wakili Mahuna aliieleza mahakama kuwa rufaa hiyo imekuja kwa ajili ya kutaja na wako tayari kupokea amri zingine za mahakama.


"Sisi tuko tayari tunaomba tarehe na wakati muafaka kwa ajili ya kusikiliza,"amesema Kweka 


Awali Mawakili wa waomba rufaa wakiongozwa na Mahuna waliwaeleza waandishi wa habari nje ya mahakama kuwa wana sababu zaidi ya 10 ambazo hata hivyo hawakuziainisha.


Oktoba 15 Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo aliwahukumu Sabaya na wenzake wawili kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kuthibitika na hatia katika makosa matatu ikiwamo unyang'anyi wa kutumia silaha.


Rufaa hiyo inatokana na shauri la awali la unyang'anyi wa kutumia silaha lililokuwa namba 105, 2021, lililokuwa likiwakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad