Sakata la GSM lafikishwa Serikalini




Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Sanaa, Utamadunia na Michezo imetoa kauli kuhusu sakata la Kampuni ya GSM kudhamini klabu zaidi ya moja katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Baadhi ya wadau wa soka nchini wameishutumu kampuni ya GSM kama chanzo cha kuharibu mchezo wa soka, kutokana na Udhamini/Ufahadili aliowekezwa kwenye baadhi ya klabu za Soka Tanzania Bara.

Waziri mwenye dhamana Innocent Bashungwa amesema Serikali itatoa ufafanuzi wa kina kuhusu sakata hilo, hivyo wananchi wanapaswa kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki ambacho sakata hilo limepamba moto mitandaoni.

Bashungwa amesema katika suala la Udhamini/Ufadhili wa GSM watu wasitie shaka nalo kwa kuwa kama ni sheria za mpira zipo, hivyo endapo kutaonekana kuwa na mambo tofauti wahusika watawajibishwa.


 
“Ukiachilia mbali TFF pia tuna Baraza la Michezo (BMT) ambalo lipo karibu katika kusimamia sheria hizo, hivyo sioni na wala wananchi wasiwe na shaka katika hilo kwani kama kutatokea ukiukwaji wowote hawatasita kuchukua hatua kwa muhusika” amesema Waziri Bashungwa.

Udhamini/Ufadhili wa GSM kwenye klabu zaidi ya moja katika Ligi Kuu, inatia shaka huenda ikaleta uchochezi wa upangaji matokeo ama kutoa ushawishi kwa waliodhaminiwa wacheze kwa namna ipi, pale wanapokutana na timu inayoonekana kuwa kikwazo katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara Zilizodhaminiwa/Kufadhiliwa na kampuni ya GSM ni Young Africans, Coastal Union na Namungo FC huku kampuni hiyo ikitajwa kuhusika katika suala la usafiri wa Biashara United kwenda Libya, japo kuwa safari hiyo haikufanikiwa.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad