Idadi ya Vituo vya Afya nchini vimeongezeka na kufikia 8461 tofauti na ilivyokuwa mwaka 1961 wakati Tanganyika inapata uhuru.
Kwa mujibu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1961 kulikuwa na vituo vya afya 1323, ambapo hospitali zilikuwa 113, zahanati 1188 na vituo vya afya 22 pekee.
Aidha mpaka sasa vituo vya huduma za afya vimeongezeka ambapo zahanati zimefikia 7163, vituo vya afya 929 na hospitali 369.
“Tumeongeza madaktari mwanzo daktari mmoja alikuwa anawahudumia watu 25000 lakini mpaka miaka 10 baadaye daktari mmoja anahudumia watu elfu 20,”amesema Rais Samia.