"Hairuhusiwi kwa Klabu, Mchezaji au Mwamuzi kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na Mdhamini wa Ligi bila ruhusa ya TFF kuhusu masuala yanayohusu mkataba wa udhamini, yoyote atakayekiuka atafungiwa kipindi kati ya miezi mitatu na kumi na mbili au faini ya shilling laki tano"
Mwisho wa kunukuu✍️
Sasa turejee kwenye hoja ya msingi, huyu pichani ni Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM ambaye pia ni Kiongozi wa Yanga ambao pia wanaidhamini Yanga na huyo pia kupitia Kampuni hiyo wanadhamini Ligi
Ukipitia Kanuni juu unaona mgongano wa kimaslahi kwakuwa Yanga na GSM wanawasiliana moja kwa moja hivyo fair ipo wapi kwa Klabu zingine ambazo zitapaswa kutekeleza mkataba huo??
Ni lazima kukaa kwenye roundtable kama Simba wanavyoiomba Shirikisho, Watu wajue mkataba unatekelezwa vipi