Shaffih Dauda "Nina Miaka 15 Kwenye Mpira Ndio Maana Nazungumza, Kinachoendelea ni Kujichoresha Mbele ya Wawekezaji"


 Kwanini DIGALA nazungumza sana?👇🔥

@shaffihdauda_ Nina miaka zaidi ya 15 kwenye game sio mingi na sio haba hivyo najua impacts za siasa za mpira kwa taswira ya mpira wetu mbele ya Wawekezaji

Nipo kwenye hii industry ya mpira, kuanzia biashara na kuzunguka nchi nyingi za kimpira duniani, si haba nafahamu vingi kwa kiasi chake

Kinachoendelea ni kujichoresha mbele ya Wawekezaji ambao huenda walitamani kuja kwenye mpira wetu haswa wa nje ya nchi, Business is all about image building

Ukishaharibu reputation yako inachukua muda kuirejesha, siasa kama hizi umeharibu mpira wa Kenya mpaka kesho, siasa hizi iliwaangusha Uganda, hatutaki kujifunza?

Kupitia sakata kama hili ambalo ni la pili kubwa ndani ya Mwaka mmoja inaonesha changamoto kwenye mfumo wa uongozi, mfumo wa uwajibikaji na uwazi wa kimkataba

Kupitia sakata hili ambalo mnaliona dogo linaweza hata kuathiri reputation ya Muwekezaji ambaye ni GSM, mmeshawahi kumfikiria GSM yeye ni Mfanyabiashara na mtaji wake ni Watu

Hamuoni kwa songombingo kama hizi mnamuharibia? Hamuoni mnamchonganisha na Simba? Mpira ni siasa Kali sana sana, jitahidini sana kulisimamia suala hili kwa weledi na unyenyekevu mkubwa, mifano ipo

Kama suala lolote lile kwenye Kanuni halipo basi njia pekee ni kukaa mezani

Sina chuki na GSM kwakuwa ni Wafanyabiashara kama Mimi

Sina shida na TFF au TPLB ni sehemu ya familia yangu

Busara iwaongoze kwenye hili

Shafih Dauda✍️

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad