Shaffih Dauda "Ni Wakati Sasa wa SIMBA Kusikilizwa Hata Kinafiki"




Wakati sisi wengine tunapambana kuhitaji kuwepo kwa safe ground ya maelewano kati ya TFF na Simba kutokana na kinachoendelea tukaonekana watatanishi

Propaganda zikapewa nafasi kubwa sana kuliko reality iliyopo mezani, ila tulifahamu vyema itafika wakati ule ukweli mchungu utapaswa kuonekana ambao ni huu

Zimefanywa kila aina ya propaganda na kashfa lakini zikiisha tu Watu wanarejea kwenye hoja ya msingi, mwisho taswira iliyojengwa ya Ligi inaharibika kisa kitu kidogo sana

Duniani kote hakuna vita iliyowahi kuisha kati ya Shirikisho au Bodi dhidi ya Klabu kubwa pasipo na kurejea mezani na kujadiliana, simply ni kuwa Wana mtaji wa watu ambao ni Wadau wa mpira

Wakati Bodi ya Ligi ya Hispania REFF inapitisha kuuzwa kwa haki za matangazo ya TV za klabu kwa miaka 50 kuelekea Kampuni ya Uarabuni, miamba Barcelona na Real Madrid walisimama, ikaisha kwa maridhiano

Zile zama za 'Umwamba' zimepitwa na wakati, unapotaka kufanya jambo Kila Mtu atareason, kwa hoja za msingi na kupima Uhalali wa jambo hilo, kwakuwa TFF, TPLB na Klabu wote ni familia ya mpira wa miguu

Tunapata tabu hii kwakuwa TPLB ambaye ndie chombo cha klabu hakiziishi interests za Klabu, tunapata tabu hii kwakuwa TFF ambao ni Watu wa Football Development wanataka bodi iwe sehemu ya kamati yao

Simba anaonekana leo hii yupo mbele ila kinamna yoyote naamini anapokea support ya hata klabu zingine ambazo kwa namna moja ama nyingine haziwezi tu kusema, sio kwamba hawataki pesa ila haziendani na mileage wanayotoa

Iliwahi Yanga kuondoka uwanjani na wakasikilizwa na sasa ni wakati wa Simba kusikilizwa hata 'kiunafki' lazima muwasikilize kwakuwa wanajua wanachofanya na wanasimamia wanachokiamini

Ogopa sana ukisikia Mashabiki na Wanachama wa timu wakisema "Bora tushuke"

Mwisho wa propaganda ni mwanzo wa ukweli ✍️

By Shaffih Dauda
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukikutana na club imara kila jambo linaenda kwa ustandard

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad