Simba yafunguka afya za wachezaji



WAKATI afya za wachezaji wa Simba ikielezwa kuendelea vema kutokana na kukabiliwa na changamoto za homa, mafua na kikohozi, wachezaji 15, benchi la ufundi, madaktari na wafanyakazi wa Mtibwa Sugar nao wamekumbwa na ugonjwa huo.

Klabu ya Azam nayo imeripoti baadhi ya wachezaji wake kupatwa na tatizo hilo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wanaendelea vizuri, lakini bado wapo kwenye uangalizi wa madaktari pamoja na wataalamu wa afya hadi hapo watakaporejea kwenye hali yao ya kawaida.

"Wachezaji wetu wanaendelea vizuri kwa sasa, lakini bado wapo kwenye uangalizi wa madaktari wa wataalamu wa afya hadi pale watakaporudi kwenye hali zao za kawaida," alisema.

Aidha, alisema wachezaji wao wanaendelea na mazoezi kwa sababu haiwezekani wakakaa bila kucheza, labda benchi la ufundi tu ambalo nalo pia lilikumbwa na changamoto hiyo.

"Huu ni ugonjwa, nashangaa watu wanaongea vitu wasivyovielewa, kwa hali yoyote haiwezekani Simba ambayo inatoka Dar es Salaam, Tanzania kwenda kucheza na Misri, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na timu kubwa kama Al Ahly na zingine, wakati mwingine inashinda nje ya nchi, leo hii iogope kwenda kucheza na Kagera Sugar au Tabora na KMC?" Alihoji Mangungu.

Mechi ya Simba dhidi ya Kagera Sugar iliyopaswa kuchezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera, iliahirishwa na Bodi ya Ligi kutokana na wachezaji 16 wa Simba kuugua.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad