Mwenyekiti wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi, Aimane Duwa amesema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na kuweka wazi timu zilizothibitisha ushiriki wao ni kumi mpaka hivi sasa.
Timu hizo ni Mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Klabu ya Yanga SC, Makamu bingwa, SimbaSC, Azam FC na Namungo FC kwa Upande wa Tanzania Bara ilhali KMKM, Mlandege, Taifa Jang’ombe, Selem View, Marine City na Yosso Club kwa upande wa timu kutoka Visiwani Zanzibar.
Mashindano hayo yanayotaraji kuanza Januari 2, 2022 visiwani Zanzibar kwa mfumo wa makundi mawili, A na B huku Vinara na washindi wapili watafuzu kucheza fainali na bingwa ataondoka na kitita cha shilingi milioni 25 na milioni 15 kwa mshindi wapili