Story Time: Amfuata Mwanamke Sweden Kutoka India kwa Baiskeli



Pradyumna Kumar "PK" Mahanandias alizaliwa mwaka 1949 katika kijiji kimoja huko India kwenye moja ya matabaka ya kihindi ya chini kabisa (untouchables) kwahiyo hakuwa na tumaini la kutoka kwenye maisha ya ubaguzi na umaskini.

Ni kawaida Kwa wahindi kuita wanajimu watoto wanapozaliwa. Mnajimu alivyoitwa alisema huyu atakuwa mtu wa Sanaa ya uchoraji. Akikua hatachaguliwa mke kama watu wengine huko India. Huyu mtoto mke wake atatoka nchi ya mbali na atakuwa na nyota ya Taurus, atakuwa mmiliki wa msitu na atakuwa mwanamuziki anayecheza filimbi (flute).

Kweli PK alikuwa mchoraji mzuri hadi akapata scholarship kwenda kusomea chuo Cha Sanaa huko India. Kwa miaka mitatu alikuwa akikaa mitaani na kuchora watu na kupata pesa. Lakini hiyo ilikuwa hairuhisiwi kwahiyo saa zingine polisi walikuwa wanamchukua wanamweka nje ya kituo Cha polisi akae hapo.

Huko alikutana na watu wengi matajiri na maarufu kama Mahatma Gandhi.

Jioni moja ya mwaka 1975, mwanamke mwenye nywele ndefu za njano (blonde) na macho makubwa ya mviringo ya blue alimfuata akamuomba amchore. Anasema mwanamke yule alivyomsogelea alikosa nguvu hawezi kuelezea.

Akasema huyu lazima nimtendee haki kwa urembo wake. Akajaribu kumchora akashindwa. Alikuwa anatetemeka. Akamuuliza huyo mwanamke unaweza kuja kesho? Huyu dada alirudi mara tatu na alichorwa mara tatu.

PK anasema alivyorudi mara ya pili alihisi huyu ndo yule mwanamke aliyetabiriwa. Akamuuliza wewe nyota yako ni Taurus? Binti akajibu ndio. Akamuuliza unamiliki msitu? Ndio. Unacheza filimbi? Binti akasema Ndio napenda kucheza filimbi na piano.

Akamwambia kwa shauku kubwa "Hii ilipangwa mbinguni! Ilikusudiwa tukutane!"

Binti akamuuliza we umejuaje? Akamwambia kama huamini nitakuonyesha Horoscope yangu iliyoandikwa nilipozaliwa. Wewe utakuwa mke wangu!

Yeye mwanamke (Charlotte) anayetoka Sweden anasema tangu akiwa mdogo alikuwa anatamani sana kwenda India. Kulikuwa na mwalimu alikuwa akiwaonyesha filamu za kihindi. Kadri alivyokua alikutana na wahindi wengi na kujifunza mengi kuhusu tamaduni zao. Aliwahi kwenda kwenye maonyesho fulani akaona ngoma ya kihindi kutoka mji aliozaliwa PK, akapumbazwa akili (hypnotized).

PK alivyomuambia kuwa atakuwa mke wake akakubali kwenda naye nyumbani kwa kina PK kuwaona ndugu zake. Anasema alijihisi nyumbani. Aliwapenda naye walimpenda. Anasema kama unaamini viumbe huzaliwa upya (reincarnation), basi yeye anaamini kabisa kuwa aliishi India zamani.

PK na Charlotte walioana na kuwa pamoja kwa muda wa wiki 3 tu kisha Charlotte akarudi Sweden. Hawakuonana mwa mwaka mmoja na nusu, zaidi ya kuwasiliana Kwa barua. Charlotte alitaka kumlipia ndege warudi wote lakini PK alikataa, alitaka ajilipie mwenyewe. Baada ya mwaka na nusu PK aliuza Kila kitu chake na kununua baiskeli.

Akaanza safari kutoka India Hadi Sweden Kwa baiskeli, umbali wa maili 4000 (6400km). Huko njiani alipata lift za maroli, alipata watu wa kumkaribisha kulala majumbani mwao, na alikuwa na "sleeping bag" aliyolalia nje akikosa pa kulala.

Alipitia Afghanistan, Iran, Turkey, Bulgaria, Yugoslavia, Germany, Austria na Denmark kufika Sweden.

Njiani aliendelea kupata barua kutoka kwa Charlotte. Alipata barua akiwa Afghanistan na Uturuki.

Anasema alikutana na watu wengi ambao walimfundisha mengi. Ilikuwa wakati wa tofauti sana maishani mwake. Ilikuwa ulimwengu wa Upendo, amani na uhuru. Shida pekee ilikuwa mawazo yake, mashaka yake.

Wamekuwa pamoja zaidi ya miaka 44 na kupata watoto wawili.

PK anasema penye nia pana njia. Uoga na mashaka ndo adui wakubwa wanaofanya maisha yetu yawe magumu. Na anasema ndoa ni muunganiko si tu wa kimwili bali wa kiroho. Na siri ya ndoa yake ya furaha ni kupaki "ego" nje ya nyumba.

Pia anasema aliamini sana utabiri wa yule mnajimu na sasa anaamini matukio yote duniani yamepangwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad