Tanzania Kupandikiza Mimba, Ukomo wa Ugumba

 


Wanawake wametakiwa kutafuta ushauri wa kitaalamu wanapokua katika wakati wa kutafuta ujauzito na kuacha tabia ya kusikiliza maneno ya mitaani au kuiga mifano ya wanawake wengine ambao wamepata Watoto kwa njia kadha wa kadha.


Rai hiyo imetolewa na daktari Edmund Isaya alipozungumza katika mahojiano maalumu na Dar24 akielezea mfumo wa kupandikiza ujauzito kwa wanawake kitaamu IVF.


“Mimi naamini kuwa vidole havifanani na wanawake hawafanani hata kila ujauzito haufanani hivyo hakikisha humuigi mtu linapokuja swala zito kama hili la IVF,” alisema Dkt. Edmund.


Alifafanua kuwa IVF kwa lugha ya kitaalamu ni In Vitro Fertilization; na kwa lugha inayoeleweka kwa haraka ni upandikizaji wa mimba kwa njia ya teknolojia ya kulitoa yai nje ya mwili wa mwanamke na kutengeneza kiumbe ambacho hurudishwa tena kwa mwili wa mwanamke ili kulea kiumbe hicho mpaka kizaliwe.


“IVF mara nyingi inafanyika pale ambapo wanandoa wamekosa kupata mtoto pamoja na kushiriki tendo la ndoa siku za urutubishaji wa yai la mwanamke lakini hashiki ujauzito. Lakini inaweza kufanyika kwa mwanamke yeyote ingawa tunafanya Zaidi kwa waliotafuta mtoto wakakosa,” alieleza dkt. Edmund.


Hivi karibuni hospitali ya Taifa ya Muhimbili ilitoa taarifa kwa umma wa watanzania kuwa itaanza kutoa huduma ya IVF kutokana na kuongezeka kwa teknolojia hospitalini hapo ikiwa ni Pamoja na misaada kutoka kwa madaktari bingwa wa nchi zilizoendelea.


Waweza kufuatilia kwa undani Zaidi maelezo ya IVF katika mahojiano hayo maalumu kupitia video hii hapa chini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad