Tanzania Yaongoza kwa Matumizi ya Bangi Afrika Mashariki




Licha ya sheria kali za kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya, tafiti zilizopo zinaonyesha kuwa Watanzania hutumia zaidi bangi kuliko wananchi wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Katika ripoti yake ya mwaka 2019, Data ya New Frontier ya Uingereza iliiweka Tanzania katika nafasi ya tano barani Afrika, huku raia wake milioni 3.6 wakisemekana kutumia bangi.

Ndani ya Afrika Mashariki, Tanzania inashika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Kenya na Uganda, ambazo zina watumiaji milioni 3.3 na milioni 2.6.

Kulingana na tafiti za New Frontier Data, watumiaji wakuu barani Afrika ni Nigeria (yenye watumiaji milioni 20.8), Ethiopia (milioni 7.1), Misri (milioni 5.9), na DR Congo (watumiaji 5).

Nafasi za Ajira zilizotangazwa leo ingia HAPA kuapply
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, alisema Novemba 2019 kuwa pamoja na kwamba serikali inapiga hatua katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, kupata ugumu wa kuzuia kilimo cha bangi katika mikoa sita ya Mara, Tanga, Morogoro, Arusha, Kagera na Ruvuma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad