TFF Wafunguka Baada ya Barbara Gonzalez Kudai Amezuiwa Kuingia Uwanjani



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikitishwa na vitendo vya vurugu vilivyofanywa na baadhi ya viongozi wa Simba kwenye eneo la kuingilia Jukwaa la Watu maalumu (VVIP) Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC na Young Africans.

Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez alifika katika eneo hilo akiwa ameongozana na Watoto watatu ambao hawaruhusiwi kuingia katika eneo hilo la VVIP.

Watoto hao ambao waliongozana naye walikuwa na Kadi za Watu wengine walioalikwa kinyume na utaratibu unavyotakiwa.

Barbara ambaye yeye aliruhusiwa kuingia alianza kutoa lugha isiyofaa kwa Ofisa wa TFF huku akirekodi video na baadaye kutupa kadi na kuondoka.

Katika hatua nyingine viongozi wengine wa Simba walifanya vurugu kwenye eneo la kuingilia baada ya kutaka kulazimisha mmoja wa viongozi kuingilia bila kadi ya mwaliko..

Tukio hilo limeripotiwa kwenye mamlaka husika zilizosimamia mchezo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad