TikTok Yaipiku GOOGLE Kama Mtandao Unaotembelewa na Watu Wengi zaidi

 


TikTok imetembelewa zaidi mwaka huu kuliko Google, kwa mujibu wa kampuni ya inayojihusisha na usalama mtandaoni, Cloudflare.


Takwimu hizo zimeonesha kuwa TikTok imeipiku Google mwezi February, March na June na imeshika nafasi ya kwanza tangia mwezi August.


Mwaka jana Google ilikuwa namba moja huku TikTok, Amazon, Apple, Facebook, Microsoft na Netflix zote zilikuwa kwenye Top 10 ya mitandao inayotembelewa na watu wengi zaidi.


Cloudfare imesema huzipata data kwa kutumia kifaa chake cha Cloudflare Radar kinachofuatilia utembelewaji wa tovuti.


Inaamini kuwa kuongezeka kwa umaarufu wa TikTok umesababishwa na janga la Covid kwakuwa uwepo wa lockdown ulimaanisha watu wengi walikuwa ndani tu na hivyo kutafuta burudani.


Hadi July mwaka huu, TikTok imepakuliwa kwa zaidi ya mara bilioni 3 kwa mujibu wa kampuni ya Sensor Tower.


Mtandao huo unaomilikiwa na kampuni ya China, Bytedance kwa sasa una watumiajia active zaidi ya bilioni moja duniani kote na namba inazidi kuongezeka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad