Dodoma. Mawaziri wawili wa Tanzania, ni miongoni mwa wahitimu 42 waliotunikiwa shahada ya udaktari wa Falsafa (Phd) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).
Mawaziri hao ni Waziri wa Madini, Dotto Biteko na Selemani Jafo ambaye ni Waziri katika Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira.
Wawili hao wametunikiwa shahada hizo katika mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga leo Alhamis Desemba 16, 2021.
Wametunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo hicho, Dk stergomena Tax. Kiongozi mwingine aliyetunikiwa shahada ya uzamivu ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde ambaye ametunikiwa shahada ya uzamivu ya umahiri ya mahusiano ya kimataifa.
Awali, Dk Stergomena alisimikwa kuwa mkuu wa chuo hicho baada ya kuteuliwa na Rais, Samia Suluhu Hassan Juni, mwaka huu, baada ya aliyekuwa mkuu wa chuo hicho, Balozi John Kijazi kufariki dunia Februari, mwaka huu.