Ugumu wa Maisha ya Ndoa na SIRI Nyingi Zilizojificha Chini ya Kapeti

 


Mambo vipi?? Wakubwa shikamoni!!

Miaka takribani 10 iliyopita nilikuwa na urafiki na wadada wawili ambao ni o level classmates wangu. Tulikuwa close sana kiasi kwamba kujua ni nani anawafatilia ilikuwa ni issue normal.

Wakati tunamaliza o level , mmoja wa rafiki yangu kati ya wale wawili alibahatika kuolewa kwa ndoa ya kanisani. Binti alikuwa ni bonge, black, haga analo, sio mrefu sana wala mfupi sana.

Miaka imeenda wakabahatika pata mtoto wa kiume, maisha yakaendelea as normal, na sasa huyo kijana wao anamiaka minne.

Kuna siku huyu rafiki wa pili akanipigia simu na kunishirikisha magumu anayopitoa shost wake kwenye ndoa, inasemekana jamaa HAJIWEZI KAMA MWANAMME (NAJUA WAKUU MSHAELEWA) hilo sio suala, suala ni kuwa jamaa ni mbishi hataki kutumia dawa kuweza kutibu tatizo lake.

Mdada anatamani kuongeza familia lakin jamaa ndohivo kimoja chali na kwa shida sana, amejaribu kwenda nae hospitali lkn jamaa ni mlokole sana hataki madawa.

Imefikia pindi huyu mkewe anataka chepuka sasa (kumbuka hii stori naambiwa na huyo rafiki yangu mwingine wa kike ambaye ni shost ake) lkn anahofia sababu hajakuzwa ktk maadili hayo.

KWA UPANDE mwingine nahic hata mwili wa huyu dada umechangia kwa kias fulani labda jamaa kukosa hamu kwa mkewe, kama nilivyosema huyu dada ni mnene lakin sasa amekuwa TIPWA TIPWA zaidi cjui unanipata navosema tipwa tipwa yani nikama yule video vixen wa ule wimbo KILA AKIPITA MINYAMAA TUU ... MWENZAKO NINAUGONJWA WA MOYOOO .... CHI CHI CHIBONGEEE CHI CHI CHIBONGEEE.

Lakini pia za chini ya kapeti ni kuwa huyu jamaa ilikuwa inasemekana hana uwezo wa kutungisha mimba, KUMBUKA mwane anamiaka minne lakini huyo mtoto kaja kupatikana miaka takribani mi3 kama sio miwili baada ya ndoa yao.

SWALI la kujiuliza kama jamaa hawezi kutungisha mwanamke mimba may be due to low sperm count, huyu mtoto waliyenae walipataje??

Au kuna jamaaa alimsaidia ili kuondoa aibu ya kuwa jamaa sio rijali??

Mie nawe hatujui.

Ndoa zinasiri nyingi usione watu wanafurahi mitaani ukahisi ndani kumetulia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad