Uhasama wa Harmonize na Diamond Wafika Pabaya



MSANII Harmonize au Harmo aliachana na Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) miaka miwili iliyopita na kuibua uhasama, lakini mwaka huu uhasama huo umefika pabaya baada ya kufichua siri kubwa kwamba utawala wa WCB ulimtaka alipe shilingi milioni 600 ili kuvunja mkataba.


Hali ilizidi kuwa mbaya mwezi uliopita na kusababisha mjadala mzito kwa wasanii hasa mashabiki wa Bongo Fleva hivyo kuufunga mwaka huu wa 2021 kwa uhasama mkubwa kuwahi kutokea.


Harmonize ambaye anamiliki Lebo ya Konde Gang na Diamond anayemiliki WCB, wamekuwa kwenye mgogoro tangu walipoacha kufanya kazi pamoja huku wafuasi wao wakitoleana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.


Lakini, katika kile kilichoonekana ni Harmonize kushindwa kujizuia, alijikuta akifichua mchakato mzima, akidai kufanyiwa mambo yasiyofaa, ikiwemo kulipishwa shilingi milioni 600 kama faini ya kuvunja mkataba wake wa miaka 10 na WCB ambao ndiyo walimtambulisha kwenye muziki.


Katika harakati za kuvunja mkataba na WCB, Harmonize alidai alilazimika kumtumia Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk John Pombe Magufuli na viongozi kadhaa, akiwemo aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.


Juhudi za kumpata Dk Mwakayembe kuzungumzia namna alivyoshughulikia sakata hilo ziligonga mwamba, kwanialipopigiwa simu alisema yupo kwenye mkutano na kutaka apigiwe baadaye, lakini alipopigiwa
tena simu iliita bila kupokelewa.


Hata alipotumiwa maswali kupitia ujumbe mfupi wa maandishi hakujibu. Harmonize alifafanua kwamba
kwamba ilibidi auze nyumba zake tatu ili apate pesa za kuwalipa WCB!


Alisema alihaha kupata pesa hizo akitaja kampuni mbili kubwa kwamba ndizo zilimpa pesa kukamilisha shilingi milioni 500.


Hata hivyo, akatakiwa aongeze shilingi milioni 100, alipewa na meneja wake, Sebastian Ndege au Jembe ni Jembe.
Harmonize alisema aliuza nyumba yake ambayo haikuwa imekamilika kwa shilingi milioni 100 kisha kampuni ya vinywaji ikampa shilingi milioni 200, halafu CRDB wakampa shilingi milioni 200 na meneja wake akampa shilingi
milioni 100.


Lakini kuna watu wanasema Harmonize alidanganya; kuna mahali hakusema ukweli. Hata hivyo, upo ukweli kwamba Harmonize alilipa shilingi milioni 500 japokuwa hilo deni WCB hawajawahi kukanusha.


Mwaka 2019, Harmonize alisema aliwalipa WCB shilingi milioni 500, lakini mwaka huu, alisema alizolipa ni shilingi milioni 600, jambo lililoibua mkanganyiko.

 

Swali la wengi ni kwamba, kwa nini Harmonize na Diamond waligombana? Jibu ni vipengele vya mkataba (contractual terms). Kuna mkataba wenye utashi wa pande zote zenye kusaini.

Mwaka 2015, Harmonize alikuwa kijana mdogo, asiye na pesa, lakini alikuwa na ndoto ya kuwa mwanamuziki mkubwa; hili alilieleza alipotembelea Global.

STORI; ELVAN STAMBULI, DAR


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad