Ununuzi wa Meli: Bosi mpya bandari matatani




MKURUGENZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Erick Hamissi, anatajwa kuwa mmoja wa watuhumiwa muhimu kwenye mradi wa kitapeli wa ujenzi wa meli tano, zenye thamani Sh.438.83 bilioni, katika eneo la maziwa na bahari ya Hindi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza, wakati mchakato wa kumtafuta mzabuni unafanyika, Hamissi ndiye alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL).

Ufisadi katika mradi wa ujenzi wa meli nchini, ulitangazwa kwa mara ya kwanza hadharani na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani, Jumamosi iliyopita, akizindua upanuzi wa gati katika bandari ya Dar es Salaam.

Kampuni ya Serikali ya MSCL, ambayo wakati huo Hamissi alikuwa Mtendaji Mkuu, ndiyo iliyosimamia mchakato wa upatikanaji wa mzabuni wa ujenzi wa meli hizo, ambao Rais Samia alisema, “mkataba wake, hauna manufaa kwa nchi.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad