Ni wazi kuwa mwanamuziki diamondplatnumz ndie msanii mkubwa kwa afrika Mashariki, licha ya kuwa mkurugenzi wa record label ya WcB pia jamaa ni Philanthropist' yaani mtu anaejitoa kwa ajili ya jamii/ mtu anae rudusha kwenye jamii kwa njia tofauti tofauti-ikiwemo kutoa msaada katika jamii.
Mapema December 07 jarida maarufu la Gluesela kupitia tovuti yake ilichapisha taarifa kuoneaha utajiri alikua nao mwanamuziki huyo nguli kutoka mbuga ya tandale, kwa mwaka 2021.Mtandao huo umemtaja Diamond kuwa na utajiri wa $10Million za kimarekani -sawa na kama Billion 21.5 fedha za kitanzania.
Miaka mi 3 nyuma pia mtandao wa Ghafla kutoka Kenya ,ulieleza kuwa Diamond aliingiza zaidi ya Billion1' katika show zake za kimataifa /yaani zile za nje ya bara la Africa.
Lakini tovuti moja ya Africa kusini imewahi eleza kuwa msanii huyo huingiza 7Million kwa siku kupitia kazi zake za muziki tu, hivyo anakusanya M730 kwa mwaka.
Diamond ndie mwanamuziki mwenye idadi kubwa ya wafuasi afrika mashariki, na tayari amefanya kazi na anafanya kazi na baadhi yavmakampuni kama Mziiki, Pepsi ,itel ,Belaire, Coral paints, Red gold, parimatch na mengine mengi ambayo yote kwa ujumla yana muingizia mkwaja mrefu sanaa.
Fununu zinadai kwamba deal lake na kampuni ya Mziiki (online streaming) ina thamani ya dolla million 5' sawa na Billion 10 za kitanzania.
Deal yake na pepsi inatajwa kuwa kubwa sana, yaani kwa taarifa za juujuu ni zaidi ya dolla 500,000, huku kampuni ya coral paint ikitajwa kumlipa zaidi ya Million 600.
Achana na hiyo juzi juzi baba yake Uncle Shamte alidai kwamba msanii huyo ananyumba zaidi ya 60 ndani na nje ya nchi ,ambazo zinamuingizi mkwanja wa kutosha, lakini Mondi pia anamiliki kampuni zake kama Wasafi media, Zoom Extra, WasafiBet, Cheka tu.
Kupitia jina lake #Diamond watu wengi wamenufaika ,na hata kupitia watu hao hao pia yeye ananufaika zaidi , itoshe kusema #diamondplatnumz ndie Mwanamuziki mwenye mkwanja mwingi zaidi Africa Mashariki.
C©✍🏾@keviiiy.iam