Wabunge 38 wa Uganda wakutwa na corona baada ya kutoka Tanzania





Safari ya wabunge wa Uganda zaidi ya 200 na wafanyakazi wa bunge 125 imeingia doa baada ya kurudi kutoka kwenye mashindano ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika mashariki, mjini Arusha Tanzania na kukutwa wana maambukizi ya uviko19.

Kwa mjibu wa msemaji wa bunge la Uganda Chris Obore amefahamisha vyombo vya habari kuwa wabunge 38 wamekutwa na mamabukizi ya virusi vya corona baada ya kupimwa na wafanyakazi 12 jumla watu 50.

Kwa mjibu wa Obore wabunge hao hawapo katika hali mbaya ya ugonjwa ndio sababu wametakiwa kujitenga majumbani mwao kwa muda wa siku 14 wakifatiliwa na watalaam wa afya.

Wabunge kutoka mataifa ya Jumuiya ya Afrika mashariki wenyeji Tanzani, Uganda, Kenya na Burundi walishiriki mashindano ya wabunge wa Jumuiya tangu tarehe 19 December 2021 mjini Arusha wengi wao wamekutwa na maambukizi.


 
Mbunge wa chama cha Jema aliyezungumuza na BBC Asuman Basalirwa akiwa nyumbani kwake alilojitenga kwa siku 7 kufanyiwa vipimo vingine, amesema walipokuwa Arusha hawakufata kanuni za watalaam wa afya za kuzuia maambukizi ya Corona kama kuvaa barakoa, kuepuka misogamano na kunawa mikono mara kwa mara.

Ameongeza kuwa wabunge wenzao wa Tanzania waliwambia kwao hakuna Corona na hivyo kupuuza kufuata kanuni za watalaam wa kudhiti corona.

Amethibitisha kuwa wabunge wa Uganda walipata maambukizi kutoka Tanzania kwani walipotoka Uganda walipimwa na kufika Arusha walipimwa kama hawana maambukizi.


Wabunge wote 200 na wafanyakazi wa bunge 125 waliosafiri kwenda Arusha hata kama hauna maambukizi ya uviko19 wameambiwa kujitenga kwa siku 14 .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad