Wanaokohoa Waongezeka, Wizara Yafafanua





Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imesema kuongezeka kwa idadi ya watu wenye dalili za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka, ni hali ya kawaida ya kila mwaka ambayo huchangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa kama ambavyo imekuwa ikitokea kwa miaka mingine iliyopita.

Taarifa iliyotolewa leo, Desemba 18, 2021 na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe inaeleza kuwa wizara pamoja na taasisi zake, zinaendelea kufuatilia kwa karibu viashiria vya hali hiyo ambapo taasisi mbalimbali ikiwemo NIMR, vyuo vikuu na wataalamu kutoka wizarani, wanaendelea kutoa takwimu na elimu kuhusu magonjwa ya milipuko.

Pia Dk. Sichalwe amewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua zote za muhimu za kujikinga na janga la Covid- 19 ikiwa ni pamoja na kuepuka misongamano, kunawa mikono kwa maji tiririka na kuvaa barakoa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad