Waandaji wa Filamu za Kitanzania ambao tayari mpo kwenye Game au Ambao bado ni wachanga ila mna ndoto ya kuwa wazalishaji wa filamu hakikisheni mnasoma sana kuhusu Filamu na Biashara yake.
Filamu sio Kimbilio la wajinga wajinga. Nchi za wenzetu zilizoendelea katika filamu, unakuta wazalishaji, waongozaji, na waigizaji wa filamu hiyo wamesoma kuhusu filamu, hakuna Ujanja ujanja kule.
Leo hii Mtanzania, Mwanadada, Seko Shamte ametangaza kuwa filamu yake "Binti" imepata nafasi ya kuoneshwa katika Platform kubwa ya Netflix, hili ni jambo kubwa sana, lakini halijatokea hivi hivi, Seko ni Msomi mkubwa tu.
Seko shamte ni Muandishi, muongozaji na Mzazishaji wa filamu. Mbali na hayo, Seko Shamte ni muigizaji mzuri, na amezaliwa na kipaji hicho, Seko ni Msomi mzuri Wa Mambo ya Fedha pamoja Na Mambo ya Media.
By Hopetyga
Seko, Amewahi kufanya kazi East Africa Tv kama Mkurugenzi wa Vipindi na katika uongozi wake vipindi bora kama Ze Comedy, Friday Night Live, Nirvana, 5 Live Vilianzishwa. Vipindi hivi ni Miongoni mwa vipindi pendwa na maarufu sana Tanzania.
Seko shamte ndio muandishi na mzalishaji wa Tamthilia ya The Team, ilikuwa inaruka Eatv kama mnakumbuka na inaelezea hasa masuala ya jinsia hasa ukombozi wa mwanamke.
Seko Shamte amewahi kutengeneza Feature Film(Filamu ndefu) iitwayo Home Coming (2015) Filamu ambayo ilifanya vizuri sana Tanzania na nje ya mipaka yetu.
So, unaweza kuona ni kwa Jinsi gani elimu imemsaidia sana seko shamte kupata mafanikio katika Filamu za kitanzania. Hivi sasa mtanzania @amilshivji anapata tuzo kubwa za filamu nje ya nchi , kwasababu kazi zake ni za kisomi na sio ujanja ujanja.