Wasanii Toka Arusha Acheni Kujibagua na Kupigania Mkoa Badala ya Taifa...Mnajibania Wenyewe

 

Juzi kwenye mkesha wa Christmas, dunia imeshuhudia magwiji wa muziki Nigeria, Wizkid, Davido, na Komredi Burna Boy, wakiungana kufanya show pamoja iliyoandaliwa na Tony Olumelu wa BOA bank. Iliashiria umoja na upendo miongoni mwa wasanii huko Nigeria. Kwa pamoja wameamua kulipigania na kuliwakilisha taifa lao vyema. Hili suala lilinitafakarisha sana hasa kuhusu sanaa ya hapa Tanzania.


Watanzania wengi waliochangia maoni kwenye post zilizohusu show ya hiyo miamba walikuwa wakiwatupia lawama kali Diamond na Alikiba. Mimi niliona wako sawa kwasababu Diamond na Kiba ni kama nembo za muziki wetu wangeweza kuhamasisha mambo yakabadilika. Ila binafsi sikupenda kujikita sana kuwalaumu hao wawili kwasababu wamefanya mambo mengi makubwa kwenye sanaa ya Tanzania. Wakati nikitafakari ndo nikakumbuka hawa wasanii kutoka Arusha. Nilipatwa na hasira kali sana kuhusiana na mienendo yao.



Wasanii wa Arusha ni wenye vipaji vikubwa pia wana exposure kubwa kutokana na kukulia kwenye kitovu cha utalii. Miongoni mwa wasanii wa mwanzo kupiga show za kimataifa walikuwa kundi la X-plastaz kutoka Arusha. R.I.P father Nelly. Hata wakongwe Chindoman na wengine ni watu wanaoijua vizuri mitaa ya mabeberu. Tatizo lililopo kwa wasanii wengi wa Arusha ni hii tabia mbaya ya kujitenga. Wao kila sehemu wanataka wawe wao tu bila kujichanganya na watu toka mikoa mingine. Hii ni tabia mbaya ya ubaguzi ambayo baba wa taifa aliichukia sana. Hayati Mwalimu Nyerere angekuwa hai angewakemea wasanii wote wanaodai wao ni wa Arachuga.


Huu upuuzi umefanya muziki wa Arusha kuwa duni sana na kuishia kuwa wasanii wa hapahapa. Na hii tabia imeota mizizi hadi kwa watu wengine ambao sio wasanii. Aliyekuwa mbunge wa Arumeru Nassari alishawahi kupanda jukwaani na kuropoka kuwa kuwepo jamhuri ya watu wa kaskazini. Mkimaliza kujibagua kwamba mmetoka Arusha mtaanza kubaguana kwamba huyu katoka Kijenge yule Kaloleni au Majengo. Watu wa Arusha tujichanganye na kusimama na watanzania wengine kama taifa moja la Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad