JESHI la Polisi Mkoa Arusha limewataka wakazi mkoa Arusha, kuchukuwa tahadhari za uhalifu na kutopeleka watoto wadogo kwenye majumba ya vileo katika sherehe za Christmas na mwaka mpya.
Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Justin Masejo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelekea mkesha wa Christmas na mwaka mpya amesema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kunakuwa na usalama maeneo yote.
“Katika mkesha mwaka mpya tumeimarisha doria za askari wa miguu na magari,lakini tunaomba Wananchi pia kuchukuwa tahadhari kutowapeleka watoto maeneo ya vilevi na madereva kuacha kuendesha magari wakiwa wamelewa” amesema.
Amesema kuwa, katika kuimarisha Ulinzi majumbani ni muhimu Wananchi wanaokwenda katika ibada kufunga nyumba ama kuacha ulinzi.
“Pia tunawataka Wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari za ugonjwa wa uviko-19 hasa kwa kuepuka maeneo yenye mikusanyiko”amesema Masejo.
Hata hivyo Kamanda Masejo amewashukuru Wakazi Mkoa Arusha Kwa ushirikiano wao na Polisi na kuweza kumaliza mwaka salama huku matukio ya uhalifu yakiwa yamepungua