Yanga kupumzisha nyota kadhaa




Yanga kupumzisha nyota kadhaa
KOCHA Mkuu wa Yanga Nasriddine Nabi amesema atawapumzisha baadhi ya wachezaji katika mchezo wao wa leo wa kombe la FA dhidi ya Ihefu.

Akizungumza na Spotileo Nabi amesema sababu ya kufanya hivyo ni kutaka kuwapa mapumziko baadhi ya nyota wake ambao wanatumika mara kwa mara kwenye mechi za ligi.

"Tuna wachezaji wengi ambao hawajacheza kwa muda mrefu nadhani hao ndio itakuwa mechi yao siyo kwamba tunadharau lakini ni moja ya mikakati tumejiwekea kutokana na wingi wa mechi ," amesema Nabi.

Kipa Djigui Diarra na baadhi ya wachezaji wa ndani akiwemo Yannic Bangala, Fiston Mayele na Feisal Salum ni miongoni mwa wachezaji ambao huenda wakapumzishwa na kutoa nafasi kwa nyota wengine akiwemo Mukoko Tonombe kuanza kwenye eneo la kiungo mkabaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad