Neno 'Match Analyst' limeanza kushika kasi huku Kusini mwa Jangwa la Sahara, mara ya kwanza kabisa kushuhudia Derby Bora kimbinu ni ya Jumapili iliyopita
Derby imeanza kuondoka kwenye uswahili na kuingia Maabara ya soka na kupika mbinu stahiki za kuisogeza mechi hii kimbinu na hesabu Kali zaidi
Kwanini Derby ile ilikuwa Bora sana? Nilipitia Tweet ya Kaka yangu @michaelmwebe alisema "When the two Coaches are too tactical, the match gets boring"
Alimaanisha mechi ikiwa na Makocha walioiva sana kimbinu basi huwa inakera, YES Kuna watu wanaamini ile haikuwa mechi Bora ila ilikuwa moja Kati ya mechi Bora sana kimbinu
Yanga walifanya assignment yao vyema, wakatumia approach waliotumia Jwaneng Galaxy kucheza dhidi ya Simba, ikisemekana baadhi ya Match Analysts wa Kizulu walifanya homework nzuri sana
Mbinu ilikuwa wacheze 'deep' kisha waipige Simba kupitia counter attacks, kwa faida ya one on one situation, kwakuwa Simba ana shida kubwa sana eneo hilo! No doubt hata Mbobezi wa kusoma mifumo kama Kocha Kaze alikubaliana na Hilo
Lakini Simba walifahamu vyema, kwakuwa Wana faida ya Pablo ambaye pia alisomea Kozi ya Match analysis! Alifanya projection ya kuhisi Yanga watatumia game ya Galaxy kama sample
Yeye alikuja na Sadio Kanoute! Huyu ndie alikuwa turning point ya mchezo wa Simba, alitaka kuwa na Kiungo mwepesi wa kulinda shape ya timu! Kisha kupitia movements zake atapunguza ukubwa wa uwanja
Simba walipopigwa press waliukunja uwanja kama ngumi, waliposhambulia waliuachia kama kitabu! Hii ilimfanya Feisal Salum kutokuwa na mechi Bora, akatoka bila hata rebound moja!
KIMBINU KUTOKA MAABARA| Simba alikuwa Bora kwenye mbinu yake, Yanga akawa Bora kwenye mbinu yake!
Well yes! When two Coaches are too tactical the match gets boring 😃
Profesa✍️