December 11, @officialalikiba na @officialzuchu walikuwa na Show Nchini kenya. Alikiba alikiwasha Naivasha, Zuchu akakiwasha Malindi.
Tuongee ukweli tu, Show hatujaiona live ila Video clip tumeziona, bila kupepesa macho, kiukweli kabisa Show ya Alikiba imebuma sana, hakuna Vibe, Raia wachache sana, yani alikuwa anaruka ruka tu.
Upande wa pili, show ya Zuchu ilikuwa ya moto sana, imagine Binti hana hata miaka miwili kwenye game, lakini anapiga show kali kuliko huyu ajayejiita King.
Waliompa Ufalme Alikiba inabidi walitafakari Upya suala hili. Hakuna haja ya Kulifumbia hili, wala Mimi sio Shabiki wa WCB lakini Ukweli lazima tuseme, ZUCHU KATISHA SANA KENYA KULIKO ALIKIBA.
Wakenya Njooni Mdondoshe Comment zenu maana nyie ndio mnamajibu mazuri kuhusu hili.