STAA wa Muziki duniani, 50 Cent ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson, alizaliwa Julai 6 mwaka 1975, ambapo katika safari yake ya muziki imempa umaarufu hadi kulifuta jina lake la kuzaliwa huku lile la 50 Cent likiwa juu.
Utajiri wake unahusishwa zaidi na dalili za mafanikio zilizoanza kuonekana februari 2003 baada ya kuibuka na albamu yake ya kwanza ya ‘ get rich or die tryin’ iliyofunika katika soko la muziki nchini Marekani.
Katika siku nne za mwanzo, albamu hiyo iliuza nakala 872 na huo ukawa mwanzo mzuri wa kumtangaza 50 Cent katika ulimwengu wa muziki kwani jina lake lilipaa si Marekani tu bali hata duniani kwa ujumla.
Kwa 50 Cent, muziki ni sehemu tu ya utajiri kwani tayari, amejiingiza katika biashara mbalimbali zilizomfanya awe juu ikiwamo michezo ya kwenye video, vitabu, mavazi na nyinginezo.
Inadaiwa kwamba kwa mwaka 2006 pekee, 50 Cent aliingiza kiasi cha dola milioni 60 zilizotokana na mauzo ya mavazi ya aina mbalimbali kupitia lebo ya G-Unit.
Hiyo ni baadhi za historia ya 50 Cent kutoka Marekani, lakini msanii huyu amekua kimya mda mrefu kimuziki baada ya mambo mengi kutokea na kupata mafanikio makubwa ya muziki hivo ameamua kuanza kujichanganya na uigizaji.
Kama ilivo ada Marekani inaongoza kwa mauaji ya wana hip hop wengi tena ya kikatili kama kupigwa risasi sasa imetambulika kwamba 50 Cent ametangaza ujio wa series inayoeleza na kufufua maovu yanayofanywa juu ya wana hip hop.
Na tamthilia hiyo itaitwa hip hop homicides ambayo itaelezea baadhi ya wana hip hop wakubwa walio uawa duniani Kama vile kifo cha Tupac na Biggiesmall.
Hata hivyo huenda 50 Cent alikuwa hapendezwi hata kidogo na pengine huenda alijaribu hata kufanya jitihada mbalimbali juu ya suala hilo lakini akashidwa sasa ameamua kuelezea vifo vya marapa kutumia series yake.