AFCON Kumekucha...Hatua ya 16 Bora Kuwaka Moto, Majirani zetu Malawi Wameupiga Mwingi Sana



BINGWA mara saba wa taji la soka kwa Mataifa ya Afrika (AFCON), Misri imefuzu katika hatua ya 16 bora, baada ya kuwafunga Sudan bao 1-0 katika mechi yake ya mwisho ya Kundi D.

Timu nyingine katika kundi hilo, Nigeria imemaliza katika nafasi ya kwanza ikiwa na alama tisa na kufuzu baada ya kuifunga Guinea Bissau 2-0.

Mataifa mengine yaliyofuzu katika hatua ya 16 ni pamoja na wenyeji Cameroon, Burkina Faso, Gabon, Senegal, Cape Verde, Guinea, Morocco na Malawi.

Ratiba ya hatua ya 16 bora ya mashindano iliyotoka jana jioni ipo kama ifuatavyo, huku hatua hiyo ikitarajiwa kuanza kesho.

Burkina Faso vs Gabon

Nigeria vs Tunisia

Guinea vs Gambia

Cameroon vs Comoros

Senegal vs Cape Verde

Morocco vs Malawi

Ivory Coast vs Misri

Mali vs Equatorial Guinea
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad