AFCON: Nigeria Watafuna Kikosi cha Moh Salah Katika Mechi ya Kundi D



Bao la Kelechi Iheanacho katika awamu ya kwanza lilisaidia Super Eagles ya Nigeria kuzamisha Misri kwenye mechi ya ufunguzi ya Kundi D. Picha: Sportvectru.com. Source: Facebook
Nigeria walitawala mechi hiyo na kuwazidi Misri maarifa katika kila idara huku kaimu kocha wa Super Eagles, Augustine Eguavoen akiwapendelea washambuliaji pilipili kama vile Moses Simon, Taiwo Awoniyi, na Kelechi Iheanacho katika safu ya uvamizi naye Joe Aribo, Wilfred Ndidi katika safu ya ulinzi.

Licha ya kutamalaki katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo, Nigeria walipoteza nafasi za wazi za kufunga mabao katika dakika za mapema.


Read also
Raila Alaani Matamshi ya Linturi 'Madoadoa' Akidai Kila Mkenya ana Haki Kuishi Popote


 
Lakini kunako dakika ya 30 ya mchezo, Iheanacho alivunja kimya akipachika mpira wavuni akitumia mguu wake wa kushoto.

Kutokana na msukumo wa kutafuta bao la kusawazisha, Misri waliekeleza kombora moja pekee langoni mwa Nigeria katika dakika ya 70 licha ya kujivunia huduma za mvamizi mahiri wa Liverpool, Mohamed Salah.

Ilikuwa hadi dakika za lala salama ndipo Salah alijaribu kufunga bao lakni kipa Maduka Okoye wa Super Eagles alimzuia.


Nigeria walishikilia ushindi wao na kupokeza Mapharao ambao ni mabingwa mara saba wa AFCON kichapo chao cha kwanza kwenye kipute cha AFCON tangu mwaka 2004 walipopigwa 2-1 na Algeria.

Mara ya mwisho Nigeria kutwaa ubingwa wa AFCON ilikuwa mnamo 2013 baada ya kupepeta Burkina Faso 1-0 nchini Afrika Kusini.

Super Eagles sasa watemenyana na Sudan kwenye mechi yao ijayo dhidi ya Sudan siku ya Jumamosi Januari 15, huku Misri wakigaragazana na Guinea-Bissau.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad