Shirikisho la Soka TFF limemshataki Polisi Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez Mashtaka hayo yamefunguliwa katika kituo Cha Polisi Osterbey Jijini Dar Es Salaam
Siku ya Al hamisi ya January 20 Barbara alipokea wito wa kufika kituoni hapo ambapo baada ya kufika aliwekwa ndani kwa saa nane kisha kusomewa shtaka lake
Shtaka linalomkabili Barbara ni kutoa lugha isiyopendeza kwa Afisa wa TFF Jacqueline Kamwamu ambae alimzuia asiingie Uwanjani katika eneo la VIP na Watoto wadogo siku December 11 2021 katika mchezo kati ya Yanga na Simba
Maneno ambayo Barbara anadaiwa kuyatamka ni Nonsense pamoja na Stupidity