Aishi na Nyoka 18 Waliokuwa Wamejificha Chini ya Kitandani Bila Kujua


Je utafanya nini ukigundua umekuwa ukilala na nyoka chumbani mwako?

Haya yalimpata mwanamke mmoja kutoka nchini Marekani ambaye amepigwa na bumbuwazi baada ya kutambua amekuwa akiishi na nyoka 18 chini ya kitanda chake.

Trish Wilcher alishtuka sana alipogundua kuna familia ya nyoka hao waliokuwa wakiishi katika chumba chake cha kulala nyumbani kwake Augusta, Georgia, Marekani. Katika posti kwenye mtandao wa Facebook, mnamo Jumatatu, Julai 12,2021 Trish alipakia picha ya wanyama hao akisema kuwa: “Angalia nyoka wote hawa waliopo katika chumba changu cha kulala. yaaani nimechanganyikiwa.”


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad