1: WANANCHI KATIKA KILELE CHA UBORA WAO🙌 WHAT A WIN.. ✊ 2 Goals.. with a Clean Sheet.. YANGA wamebeba POINTI 3 ZA THAMANI kwenye safari yao ya kupambania Ubingwa!
2: ASANTE KWA MAKOCHA✊ Melis Medo na Profesa Nabi! Tactically, walituandalia mechi nzuri ya kutazama! Kilicholeta tofauti ni 'Quality' ya wachezaji kwenye Pitch
3: Si rahisi kushinda na kutawala mechi Mkwakwani! Ibabidi Uchague moja. Mtaalamu Nabi akachagua mpango wa kushinda mechi! Kivipi?
4: Yanga ni bora kwenye kuchezea mpira! Mechi zao nyingi huanza kwenye kumiliki mpira kwa dakika kadhaa.. Pasi 10 hadi 15 mpaka goli.. Lakini kwa Coastal walichagua mpira utembee kwa kasi zaidi! Aucho & Bangala wawaka direct sana.. One & Two Touch pass.. Mpira unafika pembeni kwa kasi
5: Mpango huu ni rahisi kufanikiwa kutokana na presha wanayopata Coastal kutoka majukwaani.. ziko nyakati mabeki wao wa pembeni hupanda sana na kuharibu 'shape' yao ya ulinzi! Kama MOLOKO angekuwa na siku nzuri kazini, Yanga wangeweza kuvuna mabao/ Asist kutoka kwake
6: Niliipenda ile 'Battle' katikati ya kiwanja.. Lakini nimevutiwa mno na Pressing ya MTENJE🙌 Inahitaji Quality ya Aucho na Bangala kushinda vita ile ya Mpenje akiwa kwenye ubora ule
7: SAIDOOO✊ BRAIN YA SOKA! Uwezo wake mkubwa wa kugundua nafasi za wazi na kukimbia kuomba mpira ni silaha iliyowavuruga sana viungo na mabeki wa Coastal Union.. Bila shaka alikuwa na mechi bora sana Mkwakwani
8: NONDOO🙌 Kama kuna furaha watakayoondoka nayo mashabiki wa Coastal Union ni ule uwezo wa kijana wao MWAMNYETO! Ni Beki kiongozi mwenye nguvu, kasi na akili ya kuzuia njia za mipira!
9: Asante Farid Mussa! Kama sio mentality ya mchezaji mkubwa Saido Asingefunga lile bao! Farid alifanya maamuzi kwa ajili ya timu sio kwa ajili yake.. Akakataa Uchoyo! Akarudi na kuridia pasi yake kwa Saido mpaka ilipokubali..🙌
10: Well Done wachezaji wa Coastal Union.. Wamevuja jasho jingi kiwajani Lakini 'Quality' ya Yanga hii sio ile..👏 Asante Mshery.. Asante Djuma kwa ile krosi.. ILA YULE AKPAN ni SAMAKI MKUBWA KWENYE BWAWA DOGO
Nb: Kafungwa Coastal, Jasho wanavuja wengine 😃