1: WHAT A WIN! Unahitaji kuvuja jasho lako lote kiwanjani kushinda mechi dhidi ya Simba ukiwa pungufu zaidi ya dakika 50 kiwanjan🙌 Heshima kwa vijana wa Mbeya City
2: Well Done kocha wa Mbeya City, Mathias Lule✊ Ni wazi alifanya kazi kubwa kuijenga timu yake kisaikolojia! Mechi kubwa Lakini walibaki na umakini wao. Nilipenda sana 'reaction' yao baada ya kadi nyekundu. Ni wazi waliajiandaa na kila hali kiwanjani
3: Simba walifeli kwenye Game Plan yao na 'selection' ya wachezaji kwenye kikosi cha kwanza! Kibaya zaidi, Bao la Mbeya City likawapotezea umakini. Presha ikawa kubwa kwao kuliko Mbeya waliopungua
4: Simba waliingia kwenye mpango wa Mbeya City. Wakalazimishwa kushambulia kwa 'Long Balls'! Wakatupa mipira mingi kwenye boksi la Mbreya City Lakini 'Presha' ikawafanya wapoteze umakini kwenye kutengeneza nafasi
5: Nafikiri ni wakati wa Benchi la Ufundi la Simba kujifanyia Tathmini kwenye 'nidhamu yao'! Muda ambao unategemea watulie waje na PLAN B ndio muda wanaokuwa na presha kubwa na kubishana na waamuzi
6: WELL DONE PAUL NONGA👏 Utulivu wa viwango vya juu kabisa! Si kila straika anaweza kutulia mbele ya Manula na akipewa presha ya Inonga mgongoni na akafunga bao zuri namna ile..
7: N'godya🙌 Alianza mechi vyema kama winga wa kushoto, baada ya kadi nyekundu akashuka chini. Nidhamu kubwa kwenye kufanya jukumu la msingi la kukaba👏
8: Bocco bado ana strugle kurejesha umakini wake. First touch yake ilikuwa changamoto kubwa kwake! Ikawa rahisi kwa mabeki wa Mbeya City kuufikia mpira kutoka kwake
9: Refa Raphael Ikambi! Ziko nyakati alipatia na ziko nyakati kulikuwa na changamoto kwenye maamuzi yake! Kama ilivyokuwa kwa Mpoki, nafikiri Kanoute pia hakustahili kumaliza mechi bila Kade Nyekundu
10: Well Done Seleman Ibrahim.. Well Done Hamad Waziri..👏 Nafikiri ubora wa Dida ulikuwa kwenye vocal yake. Uzoefu wake uliisaidia kwa kiasi fulani Mabeki wa Mbeya kutopoteza umakini
Nb: Ikiwa Zanzibar ni Barcelona.. Ikirudi Bongo ni Lipuli ya Vunja Bei😃