Aliyemuua George Floyd Anakipata Cha MTEMA Kuni Gerezani

 


Askari Derek Chauvin aliyemuua George Floyd kwa sasa anayaishi matokeo ya matendo yake, akipitia maisha duni gerezani, chini ya ulinzi mkali na uhuru mdogo.


Chauvin amekuwa gerezani kwa takribani miezi 8 katika Kitengo cha Udhibiti wa Utawala, sekta ya makazi yenye vizuizi na usalama mkubwa ndani ya Kituo cha Marekebisho cha Minnesota-Oak Park Heights.


Amekuwa chini ya ulinzi mkali akiwa amezungukwa na kamera za uchunguzi katika kila hatua ya jambo lolote analojaribu kulifanya, huku wafanyakazi wa gereza hilo wakimchunguza kila baada ya dakika 30.


Kwa mujibu wa TMZ mwakilishi wa kituo hicho anasema Chauvin bado ametengwa, bila kupewa nafasi ya kufanya kazi, kuhusika na programu za elimu wala kuwasiliana na wafungwa wengine.


Mwakilishi huyo anaeleza  kuwa sio hivyo tu bali anaoga, anakula, anaenda bafuni na analala kwenye sehemu moja.


Inaelezwa kuwa anapata saa moja pekee kila siku nje ya chumba hicho kwa ajili ya mazoezi. Ingawa maisha ya gerezani ni magumu, lakini inaelezwa ugumu wa anayoyapitia Chauvin umeongezeka mara dufu kwa kuzingatia alichomfanyia marehemu George Floyd Mei 2020.


Mnamo Juni 2021, Chauvin alihukumiwa miaka 22.5  kwa mauaji ya George Floyd. Alikiri kuwa na hatia katika kesi nyingine inayomkabili ya kukiuka haki za kiraia za Floyd.


Hukumu ya kesi hiyo inaweza kumuongezea miaka 25 mingine gerezani mara baada ya kuhukumiwa ambapo atawekwa katika gereza la kudumu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad