Anusurika Kifo Baada ya kugonga Nyati wawili na kuwauwa katika Hifadhi ya Taifa Mikumi.


Mtu mmoja aitwae Thobias Mbilinyi amenusurika kifo baada ya kupata ajali kwa kugonga Nyati wawili na kuwauwa katika Hifadhi ya Taifa Mikumi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Muhifadhi Hifadhi ya Mikumi Herman Mtei amesema ajali hiyo imetokea leo January 10 2022 saa moja asubuhi katika barabara ya Morogoro - Iringa.

Amesema kuwa majeruhi huyo ambae kwa sasa amelazwa Hospitali akipatiwa matibabu alikua anaendesha gari ndogo aina ya Toyota crown namba T 995 DLF ambapo kutokana na kugonga Wanyama hao na kuwaua atalazimika kulipa faini ya milioni tisa kama fidia na adhabu za sheria za hifadhi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad