Baada ya Wadau Kudai Kajala Kapotea Mitandaoni Mwenyewe Afunguka Haya "Walitusema na Wakamaliza yote, Wakatulia Tulia"




STAA mwenye shepu yake kunako Bongo Movies, Kajala Masanja anasema kuwa, ameipisha kidogo mitandao ya kijamii ili watu waendelee na shughuli zao maana kila siku akifikiria mambo ya mitandao, yanampotezea muda wake mwingi.

Katika mahojiano Kajala anasema kuwa,kuna wakati mtu anakubali tu kuandamwa na mitandao ya kijamii, akiamini kuna muda watanyamaza na mtu utaendelea na mambo yako vizuri kama ilivyokuwa mimi kwangu huko
nyuma nilivyoandamwa na mtoto wangu (Paula).

“Kwa sasa nimeipisha mitandao kwanza iendelee na kazi zake nyingine, maana kila kukicha ilikuwa ni mimi, lakini mwisho wa siku nilikubali tu kila kitu nikaa kimya na mwisho wa siku walitusema na wakamaliza yote, wakatulia tuli,” anasema Kajala.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad