Barbara Awatuliza Mashabiki, Wanachama Simba SC Kisa Kimya Kingi Kipindi Hichi cha Usajili Tofauti na Wenzao Yanga

 


Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC umewatoa hofu Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kuhusu usajili unaoendelea katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo.


Simba SC imekua kimya katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, huku klabu nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara zikiendelea kufanya usajili na kuwatangaza wachezaji waliomaliznaa nao.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzales amesema Wanachama na Mashabiki wanapaswa kuwa watulivu katika kipindi hiki, ambapo Uongozi wao unaendelea kukamilisha mipango ya usajili wa baadhi ya wachezaji watakaoongeza nguvu kikosini.

Amesema dhamira yao kubwa ni kutaka kuwa na wachezaji wenye viwango bora ambao wataisaidia Simba SC katika kipindi hiki cha kuelekea Michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya Makundi na Ligi Kuu Tanzania Bara.


“Kutokana na mkakati wetu tuliokuwa nao viongozi kwa kushirikiana na kocha Pablo tunahitaji wachezaji walio kwenye kiwango bora na kuisaidia timu wakati huu, Niwatoe hofu katika usajili wa wakati huu tutasajili kabla dirisha halijafungwa.” amesema Barbara

Baadhi ya wachezaji ambao huenda wakasajiliwa Simba SC wapo na kikosi visiwani Zanzibar kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi, huku Kiungo kutoka Zambia Clatous Chama akihusishwa kwenye usajili wa Dirisha Dogo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad