Bashe "Hakuna Mtanzania atakayekosa chakula"



Mahindi yaliyohifadhiwa kwenye viroba tayari kwa kwenda sokoni
SERIKALI imesema kuwa pamoja na kuwepo kwa mabadiko ya tabia ya nchi yaliyosababisha kukosekana kwa mvua za uhakika, nchi ina akiba ya chakula cha kutosha. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 22 Januari, 2022 na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe jijini Dodoma alipokutana na wasambazaji wa mbolea kwa lengo la kujadili bei ambayo inampa unafuu mkulima.

Amesema kuwa hakuna Mtanzania atakayekufa na njaa kwa kuwa serikali ina akiba ya chakula cha kutosha tani 200,000 za mahindi.

Bashe amesema hawatawapa wafanyabiashara wauze tani hizo za mahindi.


Amesema serikali kupitia Halmashauri husika watafungua vituo na mahindi ambayo yatauzwa kwa bei nafuu ili wananchi wakidhi na kupata mahitaji yao.

“Wananchi ambao wanaakiba ya chakula waendelee kuhifadhi kwa sababu tunaweza tusipate chakula kama mwaka jana.

“Tathimini ya awali inaonesha uzalishaji wetu pamoja na upungufu wa mvua tulikuwa na wastani wa asilimia 125 hadi 127 lakini kipindi hiki kinaweza kushuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa,” amesema Bashe.



Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe
Waziri Bashe ameongeza kama serikali wanafahamu bei ya mbolea imepanda na msimu wa mvua za vuli zimeanza na kuna baadhi ya wakulima walitarajia kupanda licha ya upungufu wa mvua.

“Baadhi ya maeneo nchini mvua zimeanza kunyesha za masika Taarifa za Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania (TMA), zinatarajiwa mwezi huu mwishoni kutakuwa na mvua hadi Februari,” ameeleza.

Amesema maeneo ambayo ni ya mvua chini ya wastani serikali imeanza kuchukua hatua ya kuhakikisha njia mbadala za zao ambalo linaweza kuwasaidia wakulima kupata kipato.

Bashe amefafanua kuwa tayari Serikali imegawa mbegu za alizeti katika maeneo yenye mvua za wastani zaidi ya tani 1600.

Ameongeza kuwa maeneo mingine ambayo yana mvua chini ya wastani waendelee kuwasiliana na wizara kwa ajali ya kuendelea kuwapatia mbegu ambazo watazigawa kwa wakulima wapate zao ambalo litawapatia kipato na yenye kustamili ukame.

Waziri huyo amesema wametoa miongozo ya aina ya mazao ambayo yanaweza kuvumilia ukama yakiwamo mtama na mihogo katika kila mikoa.

Bashe amesema uzalishaji wa chakula umekabiliwa na bei ya mbolea na serikali inafahamu miaka ya 2015 hadi 2017 ilikuwa ikitoa ruzuku za pembejeo .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad