Binti Aliyemuua Mama yake Alitumia Blanketi Kama Sanda..Panga Lilitumika Kufanya Mauaji Lakutwa pia


Mabaki ya mwili unaotajwa kuwa wa muuguzi mstaafu Patricia Ibrock, mkazi wa Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro yamekutwa yakiwa yamezungushiwa blanket baada ya kufukuliwa kwenye shimo alipofukiwa baada ya kudaiwa kuuawa na mtoto wake kike aitwaye Wendrick Mrema.


Wataalamu kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wameondoa mabaki hayo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitaalamu kwa ajili ya kubaini vinasaba .

Silaha aina ya Panga limekutwa katika shimo liikua na mabaki ya mwili unaotajwa kuwa wa Patricia Ibrock huku kukiwa na nywele katika sehemu ya ncha.

Panga hili linadaiwa kuhusika katika kutoa uhai wa mama huyo kabla ya kufukiwa katika shimo la futi mbili jirani na nyimba yake.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad