Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA chini ya Mwenyekiti wake Profesa Sylvia S. Temu imeidhinisha matokeo ya watahiniwa 5,809 waliofanya mtihani mwezi Novemba 2021 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA). Mitihani hiyo ilifanyika katika vituo 11 vya mitihani vilivyopo Tanzania Bara na Visiwani.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Pius Maneno imebainisha kuwa matokeo hayo yanafuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 11 vya mitihani kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema mitihani hiyo ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza na ya Pili katika ngazi ya cheti cha utunzaji wa Hesabu (ATEC I , ATEC II) zenye masomo manne kila moja na ngazi ya taaluma, Hatua ya Awali/Msingi (Foundation Level) yenye masomo matano, Hatua ya Kati (intermiediate Level), yenye masomo sita na hatua ya mwisho yenye masomo manne(Final Level). Pia amesema Mitihani hii niya Kumi na tano Chini ya mfumo mpya wa elimu na Mafunzo unaozingatia weledi.
"Watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 6,446 kati ya hao watahiniwa 637 sawa na asilimia 7.6 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 5,809 sawa na asilimia 92.4. Kati ya watahiniwa hao 2,796 sawa na asilimia 48.1 ni wanawake na 3,013 sawa na asilimia 51.9 ni wanaume.
Kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo watahiniwa 202 ambao ni asilimia 3.6 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 41 sawa na asilimia 0.7 wamefaulu kwa kufaulu masomo walioyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma, wengine 708 sawa na asilimia 12.2 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza," alisema Maneno.
Pia alisema watahiniwa 961 sawa na asilimia 16.5 wamefaulu mitihani yao na kwamba watahiniwa wengine 2,559 sawa na asilimia 44.1 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi mbalimbali na watahiniwa 2,289 waliobakia sawa na asilimia 39.4 hawakufaulu mitibani yao.
Amesema katika ngazi ya awali watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 742 kati ya hao watahiniwa 65 sawa na asilimia 8.8 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali na hivyo watahiniwa waliofanya mitihani kuwa 677 sawa na asilimia 91.2.
Pia imeelezwa kuwa kati ya watahiniwa 677 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 126 ambao ni asilimia 18.6 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja huku mwingine 01 sawa na asilimia 0.1 amefaulu masomo aliyokuwa ameshindwa katika mitihani ya nyuma na wengine 119 sawa na asilimia17.6 wamefaulu mitihani waliyokuwa wamebakiza.
Imeelezwa kwa ujumla watahiniwa 246 sawa na asilimia 36.3 wamefaulu mitihani yao ambapo watahiniwa 301 sawa na asilimia 44.5 wamefaulu baadhi ya masomo katika kazi hii na watahiniwa 130 waliobakia sawa na asilimia 19.2 hawakufaulu mitihani yao.
Aidha amesema katika hatua ya Kati, waliojisaliwa walikuwa 3,379 kati ya hao watahiniwa 396 sawa na asilimia 11.7 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 2,983 sawa na asilimia 88.3. Kati ya watahiniwa 2,983 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 36 ambao ni asilimia 1.2 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 35 sawa na asilimia 1.2 wamefaulu kwa kufaulu masomo waliyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma.
Alisisitiza kuwa wengine 313 sawa na asilimia 10.5 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza, hivyo kwa ujumla watahiniwa 384 sawa na asilimia 12.9 wamefaulu mitihani yao. Watahiniwa 1,446 sawa na asilimia 48.5 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 1,153 waliobakia sawa na asilimia 38.5 hawakufaulu mitihani yao.
Katika hatua ya mwisho, waliosajiliwa walikuwa 2,076 kati ya hao watahiniwa 163 sawa na asilimia 7.9 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanua mitihani walikuwa 1,913 sawa na asilimia 92.1. Kati ya watahiniwa 1,913 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 29 sawa na asilimia 1.5 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 04 sawa na asilimia 0.2 amefaulu kwa kufaulu masomo aliyokuwa ameshindwa katika mitihani ya nyuma.
Amesema watahiniwa 236 sawa na asilimia 12.3 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza ambapo Watahiniwa 269 sawa na asilimia 14.0 wamefaulu mitihani yao huku watahiniwa 713 sawa na asilimia 37.3 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 913 waliobakia sawa na asilimia 48.7 hawakufaulu mitihani yao.
Maneno amesema kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA imetoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.