Bomu Laua Watu Watatu Msata Bagamoyo, Waliliokota Wakizani ni Chuma Chakavu



WATU watatu wamefariki dunia baada ya kulipukiwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu baada ya kuokota wakidhani ni chuma chakavu.

Akizungumza na waandishiwa habari mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema watu hao walikuwa wakijihusisha na uuzaji wa vyuma chakavu.

Alisema tukio hilo lilitokea Msata Wilaya ya Kipolisi Chalinze, ambapo watu hao waliokota chuma hicho wakidhani ni chuma chakavu kwenye eneo la Pongwe Msungura kunakodhaniwa yalikuwa yakifanyika mafunzo ya kijeshi. “Waliokufa ni Athuman Ramadhani (20), Maneno Hamisi (23) na Abdallah Rajab (21), wote wakulima wakazi wa Msata.

Ramadhan na Hamisi walikufa katika eneo la tukio na Rajab ambaye alipata majeraha makubwa alifia njiani wakati akipelekwa Kituo cha Afya Lugoba,” alisema. Kamanda Nyigesa aliwataka wauzaji na wanunuaji wa vyuma chakavu kuwa makini ili kuepuka matukio kama hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad