BREAKING NEWS: Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), leo Alhamisi Januari 20, 2022 imempitisha Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kuwania nafasi ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurithi nafasi ya Job Ndugai aliyejiuzulu.
Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kimeketi leo katika Ukumbi wa White House jijini Dodoma na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambapo Dk. Tulia ameibuka kinara kati ya wagombea 70 waliojitokeza.
Akizungumza jijini Dodoma katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Shaka Hamdu Shaka baada ya kikao hicho amesema hatua inayofuata ni jina hilo kupigiwa kura na Caucas ya wabunge wa chama hicho.