Breaking News: Waandishi wa Habari wafariki ajalini Simiyu

 


Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa jumla ya watu 11 wamefariki Dunia wakiwemo waandishi wa habari watano baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na gari dogo aina ya Hiace


Waandishi hao walikuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakielekea Ukerewe kwenye ziara maalumu ya kikazi


Akizungumza na Dar 24 Media Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Blasius Chatanda amethibitisha kutokea ajali hiyo na kutaja chanzo cha awali cha ajali hiyo kuwa ni mwendokasi


Kamanda Chatanda amesema taarifa zaidi za hali za majeruhi na idadi ya vifo vitakavyoongezeka zitatolewa baadae baada ya tathimini na uchunguzi wa kitabibu


Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Januari 11 katika eneo la Nyashomi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad