"Ni habari njema kuona maambukizi ya ugongwa huo yanapungua, nadhani ni bayana na kuna ishara kwamba idadi ya maambukizi kutokana na wimbi la nne la COVID-19 imepungua sio tu nchini Afrika Kusini bali pia kote Barani Afrika, ukiondoa maambukizi mapya tunayoyashuhudia kwenye baadhi ya Nchi za Afrika ya Kaskazini zinazokabiliwa na majira ya baridi kali".
Watalaamu kutoka WHO wamedokeza kuwa idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona barani Afrika imepungua kwa asilimia 8 na kusema wimbi la nne la Covid-19 limefika kileleni Afrika "japo makali ya wimbi la sasa yanaonekana kufifia, Bara la Afrika bado halijaondokana na janga la COVID-19 , Serikali za Nchi za Afrika zisilegeze kamba"
Download App ya Udaku Special BURE Kwenye Simu yako Upate Hizi Habari zetu Kirahisi...Bonyeza HAPA