Diva Loveness wa Wasafi Adai Ameolewa Mwaka Sasa....


MTANGAZAJI wa Wasafi FM, Diva divatheebawse amesema alishaolewa na sasa ni mwaka mmoja yupo ndani ya ndoa yake.

Kauli ya Diva inakuja baada ya kuwauliza mashabiki wake wa Facebook; “Ni habari gani imekushtua sana tangu mwaka huu uanze?” Sasa shabiki mmoja alimjibu; “Kutokuolewa mpaka leo na mahari japo umeshusha bei.”

Jibu hilo lilimfanya Diva kufichua suala la kuolewa; “Mimi ni mke wa mtu mwaka sasa au unataka nitangaze kila kitu, haya nenda serikalini wana cheti changu cha ndoa panya wewe...”

Utakumbuka kipindi cha nyuma Diva aliwahi kugonga vichwa vya habari kufuatia kudai mahari yake ni mabilioni ya pesa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad