”Duniani kuna nchi moja inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ndani yake kuna Watanzania, wito wangu kwa Watanzania ni kila mmoja huko alipo kufanya kazi kwa bidii kwa sababu tutakaoijenga ama kuibomoa nchi hii ni sisi wenyewe Watanzania,” – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 27 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
”Natoa rai kwa Watanzania kujituma na kufuata mila, desturi, Katiba ya Nchi, taratibu na Sheria za nchi tulizojiwekea. Tufanye kazi kwa bidii ili tuinyanyue nchi yetu kwani nchi haijengwi na mtu mmoja,” – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 27 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma