Eto’o: Afrika Tunadharauliana




NGULI wa zamani wa Soka wa Cmaeroon na Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo, Samuel Eto’o amesema kuwa Mataifa ya Afrika yanayo nafasi kubwa ya kushinda Kombe la Dunia kuliko Bara la Ulaya na Mabara mengine kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji awa Afrika wanaocheza huko Ulaya.

Eto’o amesema kinachoiangusha Afrika ni kudharauliana, kutopendana na kutopenda mafanikio ya wenyewe kwa wenyewe.

“Nachofahamu sisi Waafrika hatuna umoja na muungano. Tunadharauliana sisi kwa sisi. Nikwambie kitu Afrika tuna vipaji halisi kuliko Ulaya.

“Lakini kwanini hatushindi kombe la Dunia? Huwa inaniumiza sana hali iyo. Natamani nishuhudie nchi moja Afrika ikitwaa taji hilo kubwa Duniani.

Natamani sana hata kama sio Cameroon basi nchi nyingine yoyote Africa ituletee hilo taji. Ukiangalia wachezaji wetu wanaocheza Ulaya na kuzipa ushindi timu zao hawajashindwa kufanya hivyo wakiwa na timu za nyumbani.

“Unajua unahitaji kushinda mechi chache sana na kutwaa taji, mechi chache mno zinahitajika kutuletea taji nyumbani Afrika. Wachezaji wetu nategemea watajituma kadiri uwezo wao naimani tunaweza kubeba Kombe la Dunia,” amesema Eto’o.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad